August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC amvimbia Rais Magufuli

Spread the love

JOHN Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC-Mwanza) ametofautiana na kauli ya Rais John Magufuli ya kukamata vijana wanaocheza ‘pool’ wakati wa kazi, anaandika Moses Mseti.

Mongella ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku nne tu tangu ateuliwe kushika wadhifa huo na kuongeza, mchezo wa ‘pool’ ni biashara.

Hata hivyo Mongella amesema kazi ya kufuatilia vijana hao inapaswa kufanywa na wenyeviti wa serikali za mtaa.

“Kazi ya kuwakamata watu wanaocheza Pooltable ni kazi ya wenyeviti wa serikali za mitaa, ndio wanatakiwa wafanye kazi hiyo,” amesema Mongella.

Rais Magufuli mwanzoni mwa wiki hii akiwaapisha wakuu wa mikoa jijini Dar es Salaam, aliwataka wakuu hao wapya kuhakikisha wanawajibika katika nafasi zao ikiwemo kuwachukuliwa hatua vijana wanaocheza mchezo huo muda wa kazi.

Mongella amesema hayo jana wakati akizungumza na watumishi wa mkoa huo wakati akijitambulisha rasmi katika Mkoa wa Mwanza.

Mongella ambaye ni mtoto wa mbunge wa zamani wa Jimbo la Ukerewe, Getruda Mongella

kabla ya kupelekwa Mwanza, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

error: Content is protected !!