RB Leipzing inashiliki Ligi Kuu ya Ujerumani imeshikilia hatma ya klabu ya Manchester United kufuzu kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) kwenye mchezo wa leo wa mwisho wa kundi H, utakaowakutanisha timu hizi mbili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Mchezo huo utachezwa kwenye dimba la Red Bull Arena nchini Ujerumani ambapo Manchester United wanahitaji sare au ushindi wa aina yoyote ili kuweza kufuzu kwenye hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Mpaka sasa Manchester United anaongoza kundi hilo akiwa na pointi tisa, sawa na PSG ya Ufaransa waliokuwa kwenye nafasi yapili na RB Leipzing waliopo kwenye nafasi ya tatu.
Mchezo huo unaonekana kuwa mgumu kutokana na timu zote mbili kuwa na pointi sawa huku Manchester akiwa juu kwa tofauti ya mabao ya kufungwa na kushinda.
Timu yoyote itakayoshinda katika mchezo wa leo itafikisha jumla ya pointi 12 na itajihakikishia kufuzu katika hatua inayofuata na itakayosalia itakwenda kushiliki michuano ya Europa.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford nchini England, Manchester United ilibuka na ushindi wa mabao 5-0, mabao yaliofungwa na Mason Greewood, Marcus Rashford na Anthon Martial.
Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ataingia kwenye mchezo wa leo huku akikosa huduma ya washambuliaji wake wawili Edson Cavani na Anthon Martial ambao walipata majeruhi kwenye mchezo uliiopita wa Ligi Kuu nchini England.
Mchezo mwengine utakaopigwa kwenye kundi hilo utawakutanisha PSG ambao watakuwa nyumbani wakiwakalibisha Instanbul Basaksehir ambao wanashika mkia kwenye kundi hilo akiwa na pointi tatu.
Leave a comment