Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Rayvanny ‘aifuta’ Wasafi
Burudika

Rayvanny ‘aifuta’ Wasafi

Spread the love

STAA wa Bongofleva ambaye pia ni Mmiliki wa rekodi lebo ya Next level Music, Raymond Mwaikyusa ‘Rayvanny’ ameendelea kuibua minong’ono kuhusu kujiondoa kwake katika lebo Wasafi Classic Baby (WCB) baada ya kufuta utambulisho wa lebo hiyo katika akaunti yake ya Instagram. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Licha ya Wasafi kuwa lebo mama iliyomkuza kimuziki msanii huyo ambaye bado anajitambulisha kuwa yupo chini ya uongozi wa lebo hiyo, sasa amefuta Wasafi iliyokuwa ikimtambulisha kama mmoja wa wasanii wa lebo hiyo.

Maneno ambayo ameyaondoa kwenye bio yake ni yale yaliyokuwa yakisema “Signed under WCB WASAFI” na sasa bio yake hiyo imebaki kutawaliwa na maneno kama “CEO NLM MUSIC” pekee.

Kwa muda mrefu sasa baada ya msanii Harmonize kuvujisha maongezi baina yake na Rayvanny kuhusu sakata la kipindi alipokuwa akiondoka Wasafi, Rayvanny amekuwa akionekana kukosa utulivu ndani ya lebo ya Wasafi.

Mara nyingi amedaiwa kuonesha ishara za kutoka japo uongozi wa lebo hiyo kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki imekuwa ikikanusha madai hayo.

Harmonize aliporejea nchini kutoka katika ziara yake ya kimuziki nchini Marekani, alivujisha maongezi yake na Rayvanny peupe mbele ya waandishi wa habari.

Yalikuwa ni maongezi ambayo Rayvanny alisikika akimtetea Harmonize dhidi ya vitendo vya bosi wao Diamond Platnumz na kumsema Simba vibaya kwamba hakuwa anamfanyia Harmonize fadhila kipindi akiwa chini ya Wasafi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

error: Content is protected !!