January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ratiba ya uandikishaji wa wapiga kura mkoa wa Njombe

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva

Spread the love
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIATUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

 

 

 

 

 

 

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA MKOANI NJOMBE

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe, kuwa itaanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya “Biometric Voters Registration” kuanzia tarehe 16/03/2015 hadi tarehe 12/04/2015.   Aidha katika kata ya Utengule ya Mji mdogo wa Makambako Uboreshaji utafanyika kuanzia tarehe 9-15/03/2015. Uandikishaji huo utahusisha Halmashauri zifuatazo:-

Mkoa Wilaya Kata Idadi ya Vituo Tarehe Ya Uandikishaji
NJOMBE NJOMBE TC ZOTE   16/03 – 12/04/2015
  WANGING’OMBE DC ZOTE    
  NJOMBE DC ZOTE    
  LUDEWA DC ZOTE    
  MAKETE ZOTE    
  MAKAMBAKO UTENGULE 12 11-17/03/2015

 

Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa

Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:-

  • Waliotimiza umri wa Miaka 18 na kuendelea na wale wote watakaotimiza miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba, 2015.
  • Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
  • Wale wote ambao wanazo sifa za kujiandikisha lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote wa Mkoa wa Njombe kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe 16/03/2015 mpaka tarehe 12/04/2015 kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.

Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni

Kumbuka:- Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.

 

Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, S.L.P. 10923, Dar es Salaam

error: Content is protected !!