October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ratiba kuapishwa rais mpya Burundi yabadilishwa

Evariste Ndayishimiye, Rais wa Burundi

Spread the love

EVARISTE Ndayishimiye, rais mteule wa Burundi anatarajiwa kuapishwa kesho tarehe 18 Juni 2020, badala ya Agosti kama ilivyopangwa. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Tume ya Uchaguzi ya Burundi wakati wa mchakato wa uchaguzi, ilileleza kwamba rais atakayechaguliwa na wananchi, ataabishwa Agosti, ratiba hiyo imebadilishwa baada ya kicho cha ghafla cha rais wa taifa hilo, Pierre Nkurunziza.

Imeelezwa, Ndayishimiye angeweza kuapishwa iwapo Nkurunziza angekuwa hai, lakini sasa nchi haina rais na si busara kusubiri wakati huo wakati hakuna kikwazo chochote kwa sasa.

Ndayishimiye anayetokana na chama tawala wa CNDD-FDD, ataapishwa katika Mji wa Gitega ikiwa ni wiki moja baada ya mtangulizi wake kufariki dunia kwa mshtuko wa moyo.

Nkurunziza alifariki dunia tarehe 8 Juni 2020. Baada ya kuapishwa, Ndayishimiye atahudumia taifa hilo kwa kipindi cha miaka saba.

error: Content is protected !!