August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ratiba FA Cup hadharani

Spread the love

HATIMAYE ratiba ya mzunguko wa tatu wa Kombe la Chama cha Soka England (FA CUP) tayari imetolewa, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Jumla ya michezo 32 itapigwa kati ya tarehe 6-9 Januari mpaka Mei mwakani huku ikiusisha timu mpaka za Daraja la Kwanza.

Droo hiyo ambayo imepangwa na tayari imetoa mtazamo kamili wa michezo itakayo pigwa.

Bingwa mtetezi wa kombe ilo kwa sasa ni Manchester United aliyelitwaa msimu uliomalizika katika fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Wembley dhidi ya Cystal Palace. Man U ilishinda 2-1.

Man U watawakaribisha Reading katika dimba la Old Traford, huku Arsenal wakiwa ugenini na Preston North End. Manchester City watafunga safari mpaka London kuwakabili Weste Ham United.

error: Content is protected !!