Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rasmi wanawake wasio‘mabikra’ kuingia jeshini Indonesia
Kimataifa

Rasmi wanawake wasio‘mabikra’ kuingia jeshini Indonesia

Spread the love

 

JESHI la Indonesia limeondoa rasmi sharti lililodumu kwa miongo kadhaa la ‘ubikra’ kwa mabinti wanaotaka kujiunga na jeshi la nchi hiyo. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDACo … (endelea).

Kwa miaka mingi ili binti ama mwanamke ajiunge na Jeshi la nchi hiyo, alilazimika kufanyiwa vipimo vya ‘ubikra’ kabla ya kuruhusiwa kujiunga, ikiwemo kuingizwa vidole katika sehemu zake za ukeni.

Sharti hili lilikuwa la lazima, lakini lilikosolewa vikali na wanaharakati likitajwa kama ni la kudhalilisha na kunyima haki ama kuzima ndoto za wanawake wa nchi hiyo wanaotaka kuwa wanajeshi lakini hawana bikra.

Zoezi hili la kupima ubikra wakati mwingine hufanywa mpaka kwa wanawake walio katika hatua na umri wa kuolewa, na kwa anayekataa huondolewa kwenye mchakato wa kuingia jeshini.

“Vipimo vya ubikra” ni uyanyasaji wa kijinsia. Hizi sera lazima ziondolewe, “alisema Andreas Hazorno, Mtafiti kutoka Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch nchini Indonesia.

“Kawaida katika kufanya vipimo hivi huwaingizia vidole viwili kwenye sehemu zao za siri kuchunguza kama amewahi kuingiliwa ama kufanya mapenzi na mwanamume,” alisema.

Wanawake wengi waliozungumza na shirika hilo wanasema, zoezi hilo la kupima kwa kutumia vidole ni la maumivu mno na wasingependa kulisikia.

Kilio cha watetezi hawa na wanawake wa Indonesia, kimesikika na Jeshi limeamua kufuta sharti hilo, na sasa wanawake ama mabinti wanapimwa kwa vigezo vingine ikiwemo afya na uwezo wao wa kuhimili shughuli za jeshi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Kimataifa

Uganda yaanza kuchimba mafuta

Spread the love  UCHIMBAJI wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza...

Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love  MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika...

error: Content is protected !!