October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rashford atunukiwa tuzo ya Heshima na chuo kikuu

Spread the love

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford, ametunukiwa tuzo ya juu ya Udokta wa heshima, iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Manchester kutokana na harakati zake za kusaidia jamii. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Hafla ya kutunukiwa tuzo hiyo ya juu, lifanyika jana Jijini Manchester kwenye Dimba la Old Trafford na kuhudhuliwa na aliyekuwa kocha klabu hiyo Sir Alex Fergusson.

Rashford ametunukiwa tuzo hiyo, mara baada ya harakati zake za kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, kupatiwa vyakula mashuleni kuwagusa watu wengi tokea mwaka 2020.

Tamko rasmi la kumtunuku Udokta huo wa heshima lilitoka Julai 2020, licha ya kushindwa kufanyika hafla hiyo kutokana na mlipuko wa ugonnjwa wa uviko 19.

Kupitia tuzo hiyo Rashford akiwa na miaka 23, ameweka rekodi ya kuwa mtu mwenye Umri mdogo kutunukiwa tuzo hiyo ya juu ya heshima kwenye chuo Kikuu cha Manchester.

error: Content is protected !!