Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Ranieri kumrithi Jokanovic Fulham
Michezo

Ranieri kumrithi Jokanovic Fulham

Claudio Ranieri
Spread the love

MKUFUNZI wa zamani wa Leicester City, Claudio Ranieri ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Fulham inayoshiriki Ligi Kuu ya England mara baada ya kumtimua aliyekuwa kocha wao Slavisa Jokanovic, kutokana na matokeo mabovu ya timu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Ranieri amesema kuwa ni heshima kukubali mwaliko wa mmiliki wa klabu hiyo Shahid Khan na nafasi ya kuiongoza Fulham ambayo ni klabu kubwa kihistoria.

“Malengo makubwa ya Fulham hayapaswi kuishia katika ligi kuu nchini England,” alisema Ranieri.

Ikumbukwe Ranieri ndiyo kocha pekee aliyeiongoza Lecester City kutwaa taji lao la kwanza la Ligi Kuu England katika msimu wa mwaka 2016, akiwa na kikosi ambacho hakikughalimu kiasi kikubwa cha fedha kwenye usajiri.

Fulham ambayo kwa sasa inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kupoteza michezo tisa kati ya 12 waliocheza na kuruhusu mabao 31, licha ya mmiliki wa klabu hiyo Shahid Khan kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye usajili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!