Thursday , 28 March 2024
Makala & Uchambuzi

Rangi ya CCM ni ile ile

Viongozi wa CCM wakiongoza Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM
Spread the love

WAKATI wa Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005, alianza kwa makeke yaliyomsisimua kila Mtanzania.Anaandika Mhode Mkasimongwa … (endelea).

Moja ya makeke hayo ni semina elekezi kwa viongozi aliowateua toka mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.

Semina hizi zilifanyika Hoteli ya Ngurudoto mkoani Arusha. Kila mmoja aliona jinsi ajenda za maendeleo zilivyoanza kuwekewa mikakati ya utekelezaji.

Vipaumbele vya serikali ya awamu ya nne wakati huo vilielekezwa kwenye sekta ya elimu na kilimo.

Rais Kikwete alibainisha wazi ajenda hizo mbili ndizo zinazoweza kututoa mahali tulipo kwa vile ndio silaha pekee za kujenga jamii yenye hoja na kuzitekeleza kwa maarifa.

Kwa kufanya hivyo nchi yetu ingeweza kupambana na maadui wakubwa wakiwemo ujinga na umasikini. Swali la kujiuliza nani aliyeshinda, ni Rais Kikwete ama ujinga na umasikini? Tunayo majibu.

Awamu ya Tano nayo ikaingia kwa makeke yale yale, tena safari hii kila kukicha unatega sikio kuona nani mwiba umemkwama.

Rais John Magufuli akienda Mwanza basi wakurugenzi, wakuu wa wilaya, makatibu na watendaji wengine tumbo joto.

Haikuwa habari tena kusikia fulani katumbuiwa, wimbo ukaimbwa kwamba ni kuvunja njia za ufisadi zilizomea wakati wa utawala wa Rais Kikwete.

Wengi walianza kuamini kuwa, Mfalme Suleiman kaibukia Tanzania, lakini kilichotokea kwenye Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kimewaacha hoi Watanzani.

Si kwa kuwa ni jambo jipya, hapana lakini jinsi Sh. trilioni 1.5 zilivyotumika bila maelezo yaliyoeleweka kisha jambo hili likapita kimya kimya, tena katika serikali hii?! Hili linaleta taswita kwamba, CCM ni mfumo kila aingiaye ataufuta.

Maswali mengi hayajajibika mpaka sasa miongoni mwayo ni je, rais anajua zilipo? Ukimya huu maana yake nini? Mbona amekuwa mpole katika hili? Waliopika kelele kuhusu zilipo amwewasikia? Ameridhika kutojua fedha hizo zilipo? Nini kilicho nyuma ya upotevu wa kiasi hiko kukibwa cha pesa?

Makala nyingi zinaandikwa kuitathmini CCM iwapo imesaidia kusukuma maendeleo na kubadili hali za maisha ya wananchi hasa wale wa kipato cha chini.

Tujiulize licha ya kutangazwa kwa kilimo kwanza na mapinduzi ya kijani, wakulima wakubwa na wadogo wameweza kubadilisha kilimo chao kwa kuzalisha ziada kuliko awali?

Kila mwaka tumekuwa tukisheherekea sikukuu ya wafanyakazi duniani lakini taifa halijahamasika kwa kiasi kikubwa kuzifanya kazi hizo kwa moyo wote. Si viongozi wala wananchi.

Baadhi  ya watumishi  wa serikali bado ni miungu watu, hawaonekani bila  ukiritimba. Lugha zao kwa wananchi ni zile za kejeli na mipasho. Wananchi hawapati majibu ya haraka kwa kero zinazowasibu husubiri bila mafanikio.

Wamekuwa wakimwinda rais hata kwa shida zinazoweza kutatuliwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa. Haya yote ni matokeo ya mfumo wa serikali ya CCM.

Sehemu nyingi kuna malalamiko ya wananchi wanaodai  wabunge, madiwani, wakuu wa mikoa na wilaya hawawatembelei wananchi vijijini.

Miradi mingi inayotekelezwa kwenye halmashauri inabuniwa na watendaji, wananchi hawashirikishwi na si kipaumbele kwao. Umangi meza ni kansa kubwa katika uongozi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miaka 28 watumishi UDSM yaliwa na nzige, madumadu

Spread the loveGEORGE Francis anasikitika; anatembea akiwa na mawazo mengi, hajui la...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nimekumbuka Samia wa miaka 3 iliyopita

Spread the loveWAKATI naandaa makala ya safu hii wiki hii, nimejikuta nakumbuka...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Hakuna fedha za Rais

Spread the loveKUNA mambo machache mazuri ya kujifunza kutoka kwa Margaret Thatcher,...

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

error: Content is protected !!