May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ramos ‘OUT’ kikosini Hispania Euro

Spread the love

KOCHA Luis Enrique amemuacha mlizi wa Reala Madrid Sergio Ramos kwenye kikosi cha wachezaji 25 cha timu ya Taifa cha Hispania kitakachoshiriki michuano ya Euro mwezi ujao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kikosi hiko kimetangazwa leo huku kukiwa hakuna hata mchezaji mmoja wa kutoka klabu ya Real Madrid inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kutoitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania toka 2004 alipoitwa kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Euro.

Pengine mchezaji huyo ameachwa mara baada ya kuandamwa na majeruhi kwenye msimu huu, kiasi cha kumfanya kukosa michezo mingi ya La Liga na timu yake ya Real madrid.

Kwenye msimu uliomalizika Ramos ameanza kwenye michezo saba akiwa na kikosi ndani ya kikosi cha Real Madrid kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Ramos kwa sasa ana umri wa miaka 35, amecheza jumla ya michezo 180 ya timu ya Taifa ya Hispania na kufanikiwa kutwaa mataji ya Euro pamoja na kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini.

Kwenye michuano hiyo inayotarajia kuanza mwezi juni 2021 Hispania imepangwa kundi E, sambamba na timu za Taifa za Sweden, Poland na Slovakia.

Luis Enrique cocha wa kikosi cha Hispania

Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hiko ni pamoja na magolikipa David De Gea, Unai Simon na Robert Sanchez.

Huku walinzi ni Aymeric Laporte, Jordi Alba, Jose Gaya, Pau Torres, Eric Garcia, Diego Llorente, Cesar Azpilicueta na Marcos Llorente, viungo Sergio Busquets, Rodri, Pedri, Thiago, Koke na Fabian Ruiz kwa upande wa washambuliaji wataongozwa na Dani Olmo, Mikel Oyarzabal, Alvaro Morata, Gerard Moreno, Ferran Torres, Adama Traore na Pablo Sarabia

error: Content is protected !!