Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rajabu: Ni wakati wa vijana kuongoza Bunge Tanzania
Habari za Siasa

Rajabu: Ni wakati wa vijana kuongoza Bunge Tanzania

Spread the love

 

MJUMBE wa Halmashauri Kuu CCM Wilaya ya Mkinga na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Baraza la vijana wa chama hicho UVCCM Mkoa wa Tanga, Hamis Rajabu (35) amejitosa kuchukua fomu ya kugombea nafasi uspika. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Rajabu amechukua fomu hiyo leo Jumatano, tarehe 12 Januari 2022, makao makuu ya CCM White House jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukabidhiwa fomu, amesema ana haki ya kuwa spika na kuonesha umma kuwa vijana wanaweza kuongoza Bunge.

Amesema tangu Bunge lilipoanzishwa mwaka 1956 alijawahi kuongozwa na spika kijana na sasa umefika wakati wa kuongozwa na kijana.

Rajabu amesema umefika wakati sasa wa vijana kushika nafasi kubwa za maamuzi badala ya kudhani kuwa wanaotakiwa kuongoza ni wazee tu.

Katika hatua nyingine Rajabu amesema iwapo chama kitampitisha kugombea nafasi hiyo na kuwa Spika atahakikisha anawafundisha wabunge jinsi ya kuchangia.

Amesema wakati wa mijadala na kuchangia kiti cha Spika kitaelekeza Bunge kazi za wabunge, naibu mawaziri na mawaziri na namna ya kuikosoa serikali na kuishauri serikali.

Aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai

Amesema lengo lake kubwa ni kuhakikisha anarudisha Bunge katika dira ya kibunge na kufuata sheria zenye kuhakikisha mhimili wa Bunge unafanya kazi kwa ukamilifu.

Aidha amesema katika uongozi wake wa kuliongoza Bunge atahakikisha kila jambo ndani ya Bunge sheria, kanuni na misingi yote inaendelea kwa kufuatia misingi.

“Kuna mikataba ambayo inaingizwa ndani ya Bunge ambayo inaingia bungeni kwa hati ya dharura na kutokana na hiyo inatakiwa kuangaliwa vizuri,” amesema Rajabu na kuongeza:

“Bunge linatakiwa kuwa la wananchi kwa kutoa usawa kwa watu wote bila kuwa na ubaguzi wa aina yoyote kwa lengo la kutenda haki kwa watu wote,” amesema Rajabu.

CCM inatafuta mrithi wa Job Ndugai ambaye tarehe 6 Januari 2022, alitangaza kujiuzulu uspika wa Bunge.

Mchakato wa uchukuaji fomu ulianza tarehe 10 hadi 15 Januari 2022, kisha taratibu zingine ndani ya chama hicho zitaendelea kumpata mgombea mmoja.

Zaidi ya wanachama 20 wamekwisha kujitokeza kuchukua fomu wakiwemo vigogo wa Bunge.

1 Comment

  • Duh!
    Huu si ubaguzi wa umri. Vijana wa leo wavivu. Ukiwauliza wamefanya nini nje ya siasa…hakuna kitu.
    Si busara kujigamba kwa ujana. Una maana Mama Samia hafai.
    Naliona tatizo lako hapa. Unadharau wazee, hekima na busara zao.
    Vijana wengi wanahongeka, na kujifanya wanajua hata kama hawajui.
    Tatizo lake una ubaguzi wa umri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!