Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais wa zamani Ufaransa jela mwaka mmoja
Kimataifa

Rais wa zamani Ufaransa jela mwaka mmoja

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy
Spread the love

 

RAIS wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na Mahakama kuu ya Paris nchini huko baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya kuzidisha matumizi ya pesa kwenye kampeni yake ya urais ya mwaka 2012. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Sarkozy aliyeiongoza Ufaransa kuanzia mwaka 2007 hadi 2012, licha ya hukumu hiyo huenda akakwepa kwenda jela iwapo atakata rufaa.

Jaji aliyetoa hukumu hiyo leo tarehe 30 Septemba, 2021, amesema Sarkozy anaweza kutumikia kifungo cha nyumbani lakini atavalishwa kifaa maalum cha kieletroniki cha kumfuatilia.

Rais huyo wa zamani kupitia wakili wake Thierry Herzog amesema atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Wakili huyo amesema; “Rais Sarkozy ambaye tumezungumza naye kwa njia ya simu, kaniomba nikate rufaa. Nitafanya hivyo mara moja kwa hiyo hii uamuzi huu hautatekelezwa.”

Hata hivyo, Sarkozy amekuwa akikanusha kuhusika na makosa yaliyokuwa yakimkabili katika kesi hiyo maarufu kama ‘Bigmalion’ iliyoendeshwa mwezi Mei na Juni mwaka huu.

Sarkozy anatuhumiwa kutumia karibu mara mbili ya kiwango cha fedha kinachoruhusiwa kisheria ikiwa ni kiasi cha Euro milioni 22.5 sawa na Sh bilioni 60.1 katika kampeni zake za kugombea muhula wa pili wa urais katika uchaguzi alioshindwa na Francois Hollande.

Awali, waendesha mashtaka walipendekeza Sarkozy ahukumiwe kifungo cha mwaka mmoja ambacho miezi sita angelitakiwa kukaa gerezani na miezi 6 mingine atumikie kifungo cha nje pamoja na kulipa faini ya faini ya euro 3,750 sawa na Sh milioni 10.

Hukumu hii imetolewa wakati ambapo Sarkozy mwenye umri wa miaka 66 alikata rufaa baada ya kukutwa na hatia mwezi Machi katika kesi nyingine ya ufisadi ambapo anadaiwa kumhonga jaji ili apate taarifa za siri kuhusu kesi ya uchunguzi dhidi yake.

Rais huyo wa zamani alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela katika kesi hiyo. Licha ya kwamba miaka miwili ilifutwa, lakini bado hajatumikia kifungo gerezani.

Sarkozy alistaafu siasa za wazi mwaka 2017 lakini bado anaendesha siasa zake nyuma ya pazia, kwa kuwa vyombo vya habari nchini Ufaransa vimeripoti kuwa anashiriki katika mchakato wa kumchagua mgombea atakaekiwakilisha chama chake Republican katika uchaguzi ujao wa urais unaotarajiwa kufanyika mwaka 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Kimataifa

Uganda yaanza kuchimba mafuta

Spread the love  UCHIMBAJI wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza...

Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love  MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika...

error: Content is protected !!