January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais wa zamani Angola arejea nyumbani baada ya kuishi uhamishoni miaka 2

José Eduardo dos Santos

Spread the love

 

RAIS wa zamani wa Angola, José Eduardo dos Santos amerejea nchini humo kimya kimya ili isizue mtafaruku hasa ikizingatiwa bado ana nguvu ya ushawishi kwa wananchi wa nchi hiyo. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya kuondoka kwenda Uhispania kwa muda wa miaka miwili.

Rais huyo wa zamani amerejea Angola tangu tarehe 14 Septemba, 2021, wakati watu kutoka familia yake, hasa binti yake Isabel dos Santos, anakabiliwa na mashitaka ya ufisadi mahakamani.

Kurejea kwa José Eduardo dos Santos kulitangazwa mara kadhaa, lakini hakuweza kutokea.

José Eduardo dos Santos, alitawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa miaka 38.

Hata hivyo, rais huyo analindwa na katiba kwamba kwa hadhi yake kama mkuu wa zamani wa serikali, katiba inazuia mashtaka yoyote ya jinai dhidi yake hadi mwaka 2022.

Aidha, mwingine José Filomeno, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa ubadhirifu wa mali ya umma huku binti yake Isabel anashukiwa katika visa vingi vya ufisadi.

Inaelezwa kuwa kurudi kwa rais huyo wa zamani kumeidhinishwa na Rais wa sasa wa Angola na waziri wa zamani wa ulinzi wa dos Santos, Joao Lourenço.

Joao Lourenço baada ya kuchaguliwa kuwa rais na kiongozi wa chama cha MPLA ambacho ni chama tawala, alianzisha mashtaka dhidi ya watu kutoka familia ya bosi wake wa zamani.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya siasa nchini humo, Olívio Kilumbo amesema licha ya kuishi uhamishoni kwa miaka miwili, kwa sababu za kiafya, José Eduardo dos Santos bado ana nguvu kubwa ya ushawishi.

“Anapendwa na Waangola wengi, kwa sababu ndiye rais wa zamani ambaye bado yupo hai. Kwa hivyo sauti yake ni muhimu nchini Angola, kwa sababu anaweza kufaulu kwa kutekeleza jukumu la ushawishi mzuri au kuzidisha mivutano,” amesema.

error: Content is protected !!