January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais wa zamani Afrika Kusini afariki dunia

Spread the love

 

RAIS wa zamani wa Afrika Kusini na mzungu wa mwisho kuiongoza nchi hiyo, Frederik Willem de Klerk amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo … (endelea)

FW de Klerk, ambaye pia alikuwa mhusika mkuu katika kipindi cha mpito cha taifa kuelekea demokrasia, alikuwa amepatikana na saratani mwaka huu, kulingana na msemaji.

FW de Klerk alikuwa mkuu wa nchi kati ya Septemba 1989 na Mei 1994.

Mwaka 1990 alitangaza kumwachia huru kiongozi aliyepinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela, na kusababisha kura za vyama vingi mwaka 1994.

Federik Willem alizaliwa tarehe 18 Machi, 1936 huko Johannesburg, Afrika Kusini, asili yake ni kaburu na alisoma sheria na kuwa wakili

error: Content is protected !!