June 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais wa Ufaransa achapwa kofi hadharani

Spread the love

 

RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amejikuta katika wakati mgumu, baada ya kupigwa kofi la uso na mwananchi, katika ziara yake ya kikazi, aliyoifanya nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Leo Jumanne tarehe 8 Juni 2021, katika mitandao ya kijamii, imesambaa video inayomuonesha Rais Macron akikumbwa na mkasa huo, alipotembelea shule moja ya hoteli iliyoko katika ji wa Tain-I’Hermitage, nje ya Jiji la Valence.

Inadaiwa tukio hilo limetokea mapema leo, wakati Rais Macron akiwasalimia wananchi walio fika kuhudhuria ziara yake, ambapo mwanamume mmoja baada ya kupewa mkono na kiongozi huyo, kama ishara ya salamu, alimnasa kofi la shavuni.

Baada ya mwanaume huyo kumnasa kofi Rais Macron, walinzi wake waliingilia kati na kumtoa kiongozi huyo eneo la tukio.

Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, watu wawili wamekamatwa kufuatia tukio hilo.

Hata hivyo, haijaelezwa sababu za mwanaume huyo kumpiga Rais Macron.

error: Content is protected !!