April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais wa Nigeria ashitakiwa mahakamani

Goodluck Jonathan, Rais Mstaafu wa Nigeria

Spread the love

SERIKALI ya Nigeria imemshitaki aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Goodluck Jonathan katika Mahakama ya Biashara ya London, kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa kampuni ya Mafuta ya Anglo-Dutch Shell na Italian Peer Eni. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Katika kesi hiyo, Serikali ya Nigeria inamtuhumu Rais Mstaafu, Jonathan pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mafuta wakati wa utawala wake, Diezan Alison-Madueke, kuvunja sheria za nchi hiyo na kuikosesha mapato.

Serikali ya Nigeria inadai kuwa, Rais Jonathan pamoja na Madueke walitoa haki ya uchimbaji mafuta kwa kampuni ya Mafuta ya Anglo-Dutch Shell na Italian Peer Eni, na kwamba thamani ya mafuta inayoonekana katika mkataba huo ni tofauti na thamani halisi ya mafuta yaliyopo katika eneo la uchimbaji.

Mahakama hiyo imeelezwa  na Serikali ya Nigeria kuwa, thamani ya mafuta ni zaidi ya dola 3.5 bilioni kiasi ambacho ni tofauti na inavyo onekana kwenye mkataba wa nchi hiyo na Kampuni za Mafuta ya Anglo-Dutch Shell na Italian Peer Eni, ambao unaonesha thamani yake kuwa ni dola 209 milioni.

Pia, Tume ya Uchumi na Fedha nchini Nigeria imesema inajiandaa kuwafungulia mashataka viongozi wengine wa zamani waliohusika na sakata hilo.

error: Content is protected !!