RAIS wa nchini Mali, Boubacar Keita amefungua kambi ya majeshi inayohusisha nchi tano za Afrika yenye lengo la kupambana na wanamgambo katika eneo la sahel mwa Afrika lililokumbwa na mashambulizi ya kigaidi., anaandika Victoria Chance.
Kambi hiyo inahusisha askari kutoka nchi ya Nigeria, Chad, Mali, Mauritania na Burkina faso ambapo pendekezo hilo la kuunda kambi lilipasishwa mnamo Julai 2 mwaka huu katika kikao kilichofanyika katika mji mkuu wa mali Bamako.
Kuundwa kwa jeshi hilo kunahitajia bajeti ya kiasi cha Dola milioni 496, ingawa hadi sasa kumepatikana Dola 127 kwa ajili ya shughuli hiyo.
Mashambulizi ya makundi ya kigaidi katika eneo la Sahel mwa Afrika, yalianza takribani miaka mitano iliyopita, sambamba na uingiliaji kijeshi wa Ufaransa ndani ya taifa hilo la magharibi mwa Afrika.
Licha ya Ufaransa kuwa na askari wengi nchini humo, imeshindwa kurejesha hali ya usalama na amani na badala yake makundi ya wanamgambo yamekuwa yakijiimarisha kijeshi nchini humo.
Leave a comment