RAIS wa Malawi Lazarus Chakwera amemvua makamu wake Saulos Chilima mamlama yote aliyokabidhiwa, baada ya kutajwa katika kashfa ya ufisadi iliyohusisha kandarasi za serikali. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini, iliwataja maafisa 53 wa sasa na wa zamani kuwa walipokea pesa kutoka kwa mfanyabiashara wa Uingereza, Zuneth Sattarkati ya mwaka 2017 mapaka 2021.
Hata hivyo makamu huyo wa rais bado hajajibu tuhuma hizo.
Hii ni kuhusiana na kandarasi 16 ambazo Huduma ya Polisi ya Malawi na Jeshi la Ulinzi la Malawi zilitoka kwa kampuni tano za Sattar, hata hivyo waliotajwa kwenye ripoti hiyo, ni pamoja na makamu war ais,mkuu wa polis ambaye amefutwa kazi.
Lakini sheria ya Malawi hairuhusu rais kumfukuza kazi au kumsimamisha kazi, makamu wake kwa vile rais huyo ni afisa aliyechaguliwa.
‘’Kitu bora ninachoweza kufanya kwa sasa, ambacho nimeamua kufanya ni kunyima ofisi yake ya majukumu yoyote, aliyokabidhiwa huku nikisubiria ofisi ithibitishe madai dhidi yake,’’rais alisema katika hotuba yake y kimataifa siku ya jumanne.
Aidha Chakwera aliungana na Chilima kumshinda Peter Mutharika, katika uchaguzi wa urais mwaka 2020, wawili hao walikuwa wameahidi kupambana na ufisadi serikalini.
Leave a comment