March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais wa Korea atupwa jela miaka 15

Spread the love

ALIYEKUWA Rais wa Korea Kusini, Lee Myung-bak amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya rushwa. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama nchini Korea Kusini ambapo pia ilimuamuru Myung-bak kulipa faini ya dola za Kimarekani 11.5 milioni.

Myung-bak alikutwa na hatia baada ya ushahidi kuthibitisha kutenda makosa hayo alipokuwa madarakani kuanzia mwaka 2008 hadi 2013.

Mwansiasa huyo wakati wa uongozi wake alipokea dola milioni 10 kutoka kwa kampuni ya Samsung kinyume na sheria.

error: Content is protected !!