Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Rais wa DARUSO alikoroga UDSM
Elimu

Rais wa DARUSO alikoroga UDSM

Spread the love

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wamemtuhumu Rais wa serikali yao, kwa kukiuka katiba na kutumia nafasi yake kufanya mambo ya hovyo badala ya kutetea maslahi ya wasomi hao ikiwamo kuwasemea waliokosa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka jana. Anaripoti Faki Sosi …. (endelea).

Wasomi hao wamesema Rais huyo Jilili Jeremiah  anatumia nafasi yake kuwalazimisha wanafunzi wenzake wakubaliane na mawazo yake binafsi ya kumpongeza John Magufuli kwa kukataa kuongeza muhula wa uongozi kutoka miaka mitano hadi saba.

Wamesema masuala hayo anayotaka Rais wa DARUSO hayawasaidia wanafunzi kutatua kero zao ikiwamo baadhi yao kukosa mikopo kwa ajili kugharamia masomo yao.

Kutokana na hatua hiyo ya Jeremiah, Bunge la wanafunzi limepanga kuitisha kikao cha dharura ili kukuanya saini za wanafunzi kwa lengo la kumvua madaraka haraka kwa kuwa ameanza kufanya mambo ya hovyo ambayo hayalengi kuwatetea wanafunzi.

Makamu wa Rais wa DARUSO, Anastazia Antony na Spika wa Bunge la wanafunzi, Deogratias Mahinyila wamempinga kiongozi huyo huku wakisema suala la kumpongeza Rais Magufuli lingetakiwa kuwa la kwake binafsi na siyo la wanafunzi wote.

Wamesema kiongozi huyo ni kada wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo angetoa pongezi binafsi badala ya kuingiza wanafunzi wote huku akijua suala hilo haliwasaidi kitu.

Katika hatua inayoonekana kuongeza mgogoro zaidi, Rais wa DARUSO, ametangaza kuwavua nyadhifa za uongozi Mawaziri wawili wa serikali ya wanafunzi ambao pia waliipinga tamko lake la kumpomgeza rais Magufuli.

Rais huyo  ametengua uwaziri wa  Matata Juma  aliyekuwa waziri wa Mikopo kwenye serikali hiyo pamoja na naibu wake Marobo Stanilaus na badala yake amemteua Gadson George kuziba nafasi ya Matata.

Amesema kuwa viongozi wa DARUSO hawakuunga mkono tamko hilo kwa sababu halikuwa zao za mjadala wa Serikali hiyo na kwamba ni matakwa binafsi ya kiongozi huyo.

“Kama mjadala wa muda wa urais katika taifa letu haukuwa mwema kama alivyodai Rais wa DARUSO, kwa nini hakuupinga hadharani huko nyuma, lakini amesubiri kupongeza msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya jambo hilo”

Matata ambaye amevuliwa madaraka  ameeleza kuwa sababu zilizosababisha kuondolewa kwenye serikali hiyo ni hatua yake ya kupinga waziwazi tamko la Rais wa DARUSO kutokana kuwa ni tamko lilojaa hisia binafsi.

Amesema kuwa  tamko lilitolewa na Rais huyo siyo la kisomi na kwamba wakati wote amekuwa akitumia vibaya nembo ya DARUSO  kwa maslahi binafsi.

Amesema kuwa wanafunzi wa UDSM wana shida ya mikopo lakini Rais hakuwahi kuyapa kipaumbele badala yake amekuwa mtu wa kupongeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

BiasharaElimu

Benki ya Exim yazindua huduma ya ‘Exim Smart Shule’

Spread the love  KATIKA juhudi za kuboresha teknolojia za kidijitali katika sekta...

Elimu

Waziri SMZ akoshwa na kazi za Global Education Link

Spread the loveSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar SMZ imesema itaendesha msako na kuzifutia...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

error: Content is protected !!