May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais wa Chad auawa

Idriss Deby

Spread the love

 

IDRIS Deby (68), Rais wa Chad ameuawa siku moja baada ya kutangazwa kushinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza, Rais Deby ameshambuliwa na waasi waliopinga ushindi wake.

Jana Jumatatu tarehe 19 Aprili 2021, Deby alitangazwa mshindi wa kiti cha urais wa Chad, baada ya kupata asilimia 79.3 ya kura.

Taarifa ya kifo hicho imetangazwa leo na Jeshi la Chad, likisema kiongozi huyo amefariki dunia kutokana na majeraha, aliyoyapata katika mapambano kati ya jeshi hilo na waasisi, ambapo yeye alikuwa mstari wa mbele kwenye mapigano hayo.

Waasisi hao walikuwa wanajaribu kuuteka Mji Mkuu wa Chad, N’Djamena, kwa lengo la kushinikiza kiongozi huyo ang’oke madarakani.

Msemaji wa Jeshi la Chad, Azen Dernendao Aguna amesema, maafisa zaidi ya 300 wa jeshi hilo, wameuawa na wengine 150 kutekwa na waasisi hao Jumamosi katika Mji wa Kanem, nje kidogo ya Mji wa N’Djamena.

Deby aliiongoza Chad kwa muda wa miaka 30, kuanzia 1990 na katika uchaguzi huo, alikuwa anasaka nafasi ya kuendelea na muhula wake wa sita wa uongozi.

Katika uchaguzi huo uliosusiwa na vyama vya upinzani, Deby alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 79.3 ya kura.

error: Content is protected !!