Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais wa Burundi atua Kigoma, JPM ampokea
Habari za Siasa

Rais wa Burundi atua Kigoma, JPM ampokea

Spread the love

EVARISTE Ndayishimiye, Rais wa Burundi amewasili mkoani Kigoma nchini Tanzania katika ziara ya kiserikali ya siku moja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Rais Ndayishimiye amewasili mkoani humo leo Jumamosi tarehe 19 Septemba 2020 asubuhi na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Kiongozi huyo wa Burundi amefanya ziara ya kwanza tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Taifa hilo Mei 2020.

Katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Rais Magufuli amempokea Rais Ndayishimiye ambapo zimepigwa nyimbo za mataifa hayo mawili na ule wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kukagua gwaride maalum.

 

Rais huyo wa Burundi amewasili nchini Tanzania baada ya kualikwa na Rais Magufuli.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Taifa, Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza uwanjani hapo amempongeza Rais Ndayishimiye kwa kuchagua Tanzania kuwa nchi ya kwanza kutembelea tangu achaguliwe.

Endelea kufuatilia MwanaHalisi Online, MwanaHalisi TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!