
RAIS wa Botswana, Dk. Mokgweets Masisi amewasilia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere, Dar es Salaam nchini Tanzania. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).
Ndege iliyombeba Dk. Masisi, imewasili uwanjani hapo saa 5 asubuhi, leo Alhamisi, tarehe 10 Juni 2021 na kupokelewa na Waziri wa Mambo Nje wa Tanzania, Balozi Liberata Mulamula.
Mara baada ya kupokelewa, msafara wa Rais Masisi unakwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam ambapo atakuwa na mazungumzo na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Rais Masisi, atakuwa Tanzania kwa ziara ya siku mbili na kesho Ijumaa, ataondoka kurejea nchini mwake.
More Stories
Msukuma: Mbowe alipa-miss Ikulu
Wabunge upinzani, CCM waungana kumpongeza Rais Samia
Dk. Mollel naye aagizwa kujibu maswali kwa ukamilifu