Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Urusi, Ukraine kukutana ana kwa ana mkutano G20
Kimataifa

Rais Urusi, Ukraine kukutana ana kwa ana mkutano G20

Spread the love

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin na Volodymyr Zelensky wa Ukraine ambao ni mahasimu kutokana na vita inayoendelea kati ya nchi hizo mbili, wanatarajiwa kukutana ana kwa ana katika Mkutano wa nchi 20 zenye uchumi mkubwa duniani G20. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu nchini Indonesia. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika taarifa iliyotolewa leo tarehe 30 Aprili, 2022 na Rais wa Indonesia, Joko Widodo amesisitiza kuwa Putin na Zelensky lazima wahudhurie.

Rais wa Ukraine

Rais Widodo amesema tayari ametuma mualiko kwa marais wote wawili.

Hata hivyo, kumekuwa na presha kutoka upande wa Marekani ambapo Rais Joe Biden ameshinikiza Urusi iondolewe kwenye mkutano huo.

Biden anaomba kuungwa mkono na mataifa mengine wanachama japo changamoto ya wazi ipo kwa China ambao wameshikilia msimamo wake wa kutokuunga uamuzi huo.

Aidha, Katibu wa habari wa Ikulu ya Marekani, Jane Psaki amesema: “Rais amekwishaweka wazi kwa umma mtazamo wake kuhusu Rais Putin kuhudhuria mkutano wa G20.

“Ni miezi sita kabla, hatuwezi kutabiri katika muda huu kwamba baadae itakuwaje, tumesilisha mtazamo wetu kwamba hatuoni kama anatakiwa kuwa sehemu ya mkutano huo iwe hadharani au kwa siri.”

Hata hivyo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha kupokea mualiko huo.

Katika taarifa yake aliyoandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ameandika: “Nilikuwa na mazungumzo na Rais Jokowi, nashukuru kwa mualiko na msaada wako katika kupigania uhuru na usalama wa mipaka ya nchi.

“Lakini hasa ikiwa ni sambamba na maadhimio ya Umoja wa Mataifa, tulijadiliana masuala ya usalama na chakula, nashukuru sana kwa kunialika kwenye mkutano wa G20.”

2 Comments

  • Marekani ni nani hata amue nani aalikwe na nani asialikwe? Hiyo ni kazi ya Rais Wadodo. Biden hana auwezo huo na dunia inapaswa ikatae kuingiliwa

  • I support participation of all G20 leaders/members because politicization of trade is not in the philosophy of globalization. I cannot remember those involved in similar adventures in recent history facing similar boycotts. .However, wars cannot be used anywhere settle disagreements. We plead for peace and a quick peaceful resolution of the fighting neighbours.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Ramaphosa akiri tatizo la umeme Afrika Kusini kuathiri sekta ya madini

Spread the love  RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema tatizo la...

Kimataifa

Idadi ya vifo tetemeko la ardhi yafikia 9000

Spread the love  IDADI ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi Uturuki: Vifo vyaongezeka hadi 4,800

Spread the love  Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi laua watu 300 Uturuki, Syria

Spread the love  WATU  300 wamefariki dunia katika tetemeko kubwa la ardhi...

error: Content is protected !!