RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky kesho Jumatano tarehe 23 Machi, 2022 anatarajiwa kuhutubia Bunge la Japan kwa njia ya mtandao.
Hotuba yake inatarajiwa kuzungumzia mashambulizi ya Urusi nchini mwake, kuomba msaada na uungwaji mkono kutoka kwa mataifa mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Kwa mujibu wa Aljazeera, hotuba ya Rais huyo inatarajiwa kutumia dakika 10 pekee na itaonesha mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa.
Rais huyo amepata nafasi hiyo baada ya Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida kukubaliana na mpango huo katika kutoa nafasi kwa Ukraine kuendelea kuomba msaada wa kimataifa kukabiliana na vita hiyo.
Tangu vita ianze tarehe 24 Februari, mwaka huu, Rais huyo wa Ukraine amekwishahutubia Bunge la Marekani, Ulaya, Canada na Israel.
Leave a comment