Tuesday , 16 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Ukraine akataa ofa ya Marekani, ni ya kuikacha nchi yake
Kimataifa

Rais Ukraine akataa ofa ya Marekani, ni ya kuikacha nchi yake

Rais wa Ukraine, Volodomyr Zelenskky
Spread the love

 

WAKATI vita kati ya Urusi na Ukraine ikizidi kushika kasi kwa siku ya tatu mfululizo, imeelezwa kuwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amekataa ofa ya Marekani ya kumsaidia kuondoka Ukraine. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Hayo yamejiri baada ya wanajeshi wa Urusi kudaiwa kuwa wameanza kuuzingira mji mkuu wa Ukraine, Kyiv kuanza jana usiku tarehe 25 Februari, 2022 na kuzidisha hali ya hatari katika taifa hilo lilipo Barani Ulaya.

Gazeti la Washington Post la Marekani limewataja maofisa wa Marekani na Ukraine ambao walisema kuwa serikali ya Marekani iko tayari kumsaidia Rais Zelensky.

Marekani ilidai imepata taarifa kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametuma vikosi vya utekaji nyara kumteka nyara au kumuua.

Hata hivyo, Rais wa Ukraine, amejibu kwamba “Mapambano yamefika. Nahitaji risasi, sio msaada wa kuondoka.”

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Associated Press Rais Zelensky amepongezwa kwa majibu yake hususani katika mitandao ya kijamii.

Rais wa Marekani, Joe Biden

Mchekeshaji na mwigizaji huyo wa zamani hapo awali alitoa hotuba ya kusisimua ambapo aliapa kuendelea kupigana, akisema: “Unapotushambulia, utaona nyuso zetu. Sio migongo yetu.”

Pia alikuwa amechapisha video ya kujipiga mwenyewe mapema jana Ijumaa ikimuonyesha yeye na wasaidizi wake wakuu katika mji mkuu, akipinga ripoti kwamba alikimbia Kyiv.

Alisikika akisema “Kuna habari nyingi za uongo mitandaoni ambazo zinadai eti ninatoa wito kwa jeshi letu kuweka silaha chini na kwamba kuna usafirishaji wa kuwaondoa watu.

“Niko hapa. Hatutaweka chini silaha zetu. Tutatetea taifa letu,” alisema Rais huyo akiwa nyuma ya Jumba la moja lililopo mji mkuu wa Kyiv.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

Habari za SiasaKimataifa

Rais Faye amteua aliyekuwa mfungwa mwenzie kuwa waziri mkuu

Spread the loveRais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ousmane Sonko...

error: Content is protected !!