Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Rais Uhuru Kenyatta ageuka ‘mbogo’ Kenya
Makala & Uchambuzi

Rais Uhuru Kenyatta ageuka ‘mbogo’ Kenya

Uhuru Kenyata, Rais wa Kenya
Spread the love

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa taifa hilo lina ‘matatizo’ na idara ya mahakama ambayo inahitaji marekebisho, anaandika Mwandishi Wetu.

Alikuwa akizungumza katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na runinga siku moja tu baada ya mahakama ya juu kubatilisha uchaguzi wake na kuagiza uchaguzi mpya katika kipindi cha siku sitini.

Rais Kenyatta alisema kuwa ataiangalia idara ya mahakama mbali na kurudia ujumbe wake kwamba atauheshimu uamuzi wa mahakama hiyo.

”Hata iwapo wewe ni mjinga jiulize hivi, matokeo ya uchaguzi wa MCA yalikubaliwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali mengi, matokeo ya maseneta na ya wabunge nayo yalitangazwa na tayari wameapishwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali.

Matokeo ya magavana yalitangazwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali ,sasa inakuwaje watu wanne wanaamka na kusema kuwa matokeo ya urais yaliyotangazwa yalikuwa na dosari.

Kivipi, kivipi? aliuliza rais Kenyatta katika Ikulu ya rais alipokutana na viongozi wa chama cha Jubilee waliochaguliwa.

Rais huyo aliyeonekana kuwa na hasira alionya kukabiliana na majaji hao wa mahakama ya juu atakapochaguliwa.

”Tuna matatizo hapa mwanzo ni nani aliyewachagua? tuna tatizo na lazima turekebishe”, alisema.

Amesisitiza kuwa japokuwa anaheshimu uamuzi wa mahakama hiyo ya juu na kwamba alikuwa tayari kushiriki katika uchaguzi mwingine huku akisema uamuzi wa mahakama hiyo ulikuwa na makosa.

”Mahakama ya juu iliketi chini ikaamua kwamba hiyo ndiyo yenye nguvu zaidi ya Wakenya milioni 15 walioamka alfajiri na kupanga foleni na kumpigia mgombea wa urais waliomtaka.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & Uchambuzi

Vijana wanavyoandaliwa kuziba pengo la ujuzi sekta ya madini

Spread the loveMOJAWAPO ya sekta ambazo katika miaka ya 2000 hazikuwa na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Lowassa: Mwanasiasa aliyetikisa CCM, Chadema

Spread the loveWAZIRI Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki Dunia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

error: Content is protected !!