September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Ufilipino hatapeleka majeshi Ukraine

Spread the love

 

NCHINI Ufilipino Rais Rodrigo Duterte amesema kuwa hatapeleka Wanajeshi wake kupigana nchini Ukraine iwapo Marekani itahusika katika mzozo huo. Inaripoti BBC (endelea).

Mataifa hayo Marekani na Ufilipino , yamekuwa na mkataba wa ulinzi wa pande zote mbili, ambao unaahidi kwamba Mataifa yote mawili kusaidiana ikiwa nchi yoyote ingeshambuliwa na mtu wa nje.

Taarifa hiyo imekuja baada ya Rais huyo, kutoa hotuba yake siku ya jana alhamisi tarehe 17 machi 2022, akimtaja Rais wa Urusi kama Rafiki yake binafsi.

Amesema ‘’Sitafanya hivyo ikiwa Wamarekani watashiriki vita hivyo , kwa nini nitume Wanajeshi wangu , sio vita vyetu kupigana,‘’ amesema Duterte katika hotuba yake.

Hata hivyo amesema kwamba ikiwa vurugu zitaendelea na vita kwa namna fulani, vifike kwake hiyo itakuwa ngumu sana kwakuwa yeye ndio Rais, “siwezi kumtuma hata mwanajeshi wangu mmoja kwenda vitani.”

Baada ya kuingia madarakani mwaka 2016 Duterte amechukua hatua za kuimarisha uhusiano na MOSCOW, huku akikosoa Sera za Usalama wa Marekani.

Aidha Duterte amesema amekutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin mara mbili mjini Moscow.

Pia alilinganisha mzozo wa Ukraine na Vita vyake dhidi ya Madawa ya Kulevya , ambayo imeshuhudiwa na maelfu ya washukiwa wa dawa za kulevya wakiuwawa wakati wa operationi za Polisi tangu mwaka 2016 .

“Putini anaua raia huko ‘’alisema “Niliua wahalifu kwa sababu ya dawa za kulevya.’’

error: Content is protected !!