RAIS wa Marekani, Donald Trump na mkewe Melania Trump, sasa wapo karantini baada ya kukumbwa na virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti BBC … (endelea).
Kabla ya Trump na mkewe kukutwa na corona, wasaidizi wake wawili walipimwa na kubainikwa kuambukizwa virusi hivyo.
Kupitia ukurasa wake wa twitter, Trump amethibitisha yeye na mkewe kukumbwa na virusi vya ugonjwa huo akisema ‘anajiweka karantini kwa siku 14.’
Pia Melania (50) kwenye ukurasa wake wa twitter ameandika.

”Kama ambavyo raia wengi wa Marekani wamefanya mwaka huu, Rais Trump na mimi tuko kwenye karantini nyumbani baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona.
“Tunaendelea vizuri na nimeahirisha shughuli zote zijazo. Tafadhali hakikisha uko salama na tutashinda changamoto hii pamoja.”
Hope Hicks (31) ambaye ni mshauri wa Trump, ndio msaidizi wa kwanza wa rais kukumbwa na virusi hivyo.
Wawili hao (Trump na Hicks) walisafiri pamoja wakati Trump alipokwenda kwenye mdahalo wa Televisheni alipokabiliana na mpinzani wake Joe Biden Jumanne wiki hii.
Leave a comment