Tuesday , 3 October 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Trump kupandishwa kizimbani
Kimataifa

Rais Trump kupandishwa kizimbani

Spread the love

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameshtakiwa katika mahakama ya wilaya ya Kaskazini iliyoko kwenye jimbo la Calfornia, kwa kutangaza hali ya dharura ili akusanye fedha za ujenzi wa ukuta ulioko mpakani mwa taifa hilo na nchi ya Mexico. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kesi hiyo imewasilishwa jana Jumatatu katika mahakama ya wilaya ya Kaskazini na muungano wa majimbo 16 ya nchini Marekani, yakiongoza na jimbo la Calfornia, ukiwa na lengo la kuiomba mahakama kuzuia matumizi mabaya ya nguvu za rais.

Mkuu wa Sheria katika jimbo la California, Xavier Becerra amedai kuwa, wanamshtaki Rais Trump ili kumzuia kutumia vibaya pesa za walipa kodi wa Marekani zilizotengwa kisheria na bunge kwa ajili ya matumizi ya watu walioko katika majimbo hayo 16.

Katika kesi hiyo, muungano huo umeiomba mahakama kutoa zuio kwa Rais Trump kutotekeleza mpango wake wa ujenzi wa ukuta hadi pale kesi itakapoanza kusikilizwa na kutolewa maamuzi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Rais Trump akiwa Ikulu ya ‘White House’ alitangaza hali ya hatari ili apate fursa ya kukusanya dola 8 bilioni kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa ukuta huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Urusi yafungua milango kwa nchi za Afrika

Spread the loveSERIKALI ya Urusi imefungua milango ya ushirikiano wa kiuchumi, kijamii...

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Putin aita vikundi vya kujitolea vita ya Ukraine

Spread the loveRAIS wa Urusi, Vladimir Putin, amefungua milango ya ushirikiano kwa...

Kimataifa

Mlipuko wa bomu waua 50 katika sherehe za Maulidi ya Mtume

Spread the loveWATU takribani 50 wamefariki dunia huku wengine 50 wakijeruhiwa katika...

error: Content is protected !!