Sunday , 3 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Trump awachefua watangulizi wake
Kimataifa

Rais Trump awachefua watangulizi wake

Spread the love

MARAIS wawili wa zamani nchini Marekani wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hali ya kisiasa nchini humo bila kumtaja kiongozi wa sasa wa taifa hilo kubwa kiuchumi duniani, Donald Trump.

Barrack Obama aliwataka wapiga kura kukataa kile alichokitaja kuwa siasa za kuwaweka watu mbali na siasa.

Aliyasema hayo katika kampeni mgombea wa chama cha Democrat anayewania wadhifa wa gavana wa jimbo la New Jersey.

Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya mtangulizi wake George W. Bush kukosoa unyanyasaji na chuki katika maisha ya kawaida ya raia wa Marekani.

Katika hotuba yake, alisema chuki dhidi ya wale wanaokupinga zimeongezwa nguvu huku maadili ya kiraia yakisahaulika.

Trump ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa mtangulizi wake bado hajatoa tamko lolote.

Marais wa zamani nchini Marekani kwa kawaida huwa nadra kutoa maoni yao kuhusu hali ya kisiasa na ilionekana kuwa makosa makubwa kwa rais aliyetangulia kumkosoa mrithi wake katika Ikulu ya White House.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za chama cha Democrat , mjini New Jersy, Obama alisema kuwa Wamarekani wanapaswa kutuma ujumbe kwa ulimwengu kwamba tunakataa siasa za kugawanywa na siasa za hofu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

Kimataifa

Papa Francis kumfukuza Kardinali anayepinga mageuzi Kanisa Katoliki

Spread the loveKIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anadaiwa kupanga kumfumkuza...

error: Content is protected !!