March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Trump atishia kuangamiza vyombo vya habari

Spread the love

RAIS Donald Trump ametangaza vita na vyombo vya habari nchini mwake kwa madai kwamba vimekuwa vikikiuka taratibu na kuonyessha ama kuandika habari kwa upendeleo, anaandika Mwandishi Wetu.

Amesema anaweza kufuta leseni za vituo vya runinga nchini mwake kutokana na kuwapo na kasoro za ukiukwaji wa tararibu.

Moja ya vitu vilivyomkasirisha Rais Trump ni pamoja na kituo cha runinga cha NBC kutangaza habari kwamba yeye aliwaagiza maofisa wake wa usalama pamoja na majenerali kuongeza kiwango kikubwa cha silaha za kinyuklia nchini humo.

Rais huyo alisema kuwa habari hiyo ilitungwa huku waziri wake wa ulinzi, Jim Mattis akisema taarifa hiyo haikuwa na ukweli wowote.

Wiki iliopita kituo cha NBC kilitoa taarifa kwamba waziri wa masuala ya kigeni nchini Marekani, Rex Tillerson alimuita Trump ‘mtu mjinga’ matamshi ambayo hayajakanushwa lakini ambayo rais huyo ameyataja kuwa habari bandia.

Wanahabari wanasema kuwa rais huyo atapata shida kufuta lesen za vyonbo vya habari. Leseni za vyombo vya habari zinadhibitiwa na tume ya mawasiliano nchini humo.

Baadhi ya makundi ya kupigania haki yanasema kuwa rais Trump anaweka mfano mbaya kwa viongozi wengine.

error: Content is protected !!