November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Trump akubali kung’oka

Donald Trump

Spread the love

DONALD Trump, Rais wa Marekani amesalimu amri mbele ya Joe Biden na sasa anajiandaa kung’oka madarakani. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Ameelekeza taasisi husika inayohusika kufanya mabadiliko ya kiuwongazi, kuanza mchakato huo kwa kushirikiana na Biden ambaye ni rais mteule wa taifa hilo.

Kwenye ukurasa wake wa twitter, Trump ameandika “haidhuru, kwa maslahi ya nchi yetu, napendekeza Emily (Emily Murphy, ofisa ofisi ya mabadiliko) na timu yake kufaya kile kinachostahili kwa kuzingatia itifaki za awali na pia nimearifu timu yangu kufanya vivyo hivyo.”

Joe Biden, Rais Mteule wa Marekani

Wafuasi wa Biden wamefurahishwa na kauli ya Trump kukubali kuondoka madarakani,”uamuzi huo ni hatua ya kiutawala ya kuanza rasmi kwa mchakato wa mabadilishano ya madaraka na mashirika husika.”

Katika uchaguzi huo uliofanyika mapema mwezi huu, Biden alitangazwa kupata kura 306 huku Trump alipata kura 232 hata hivyo, awali Trump aligomea matokeo hayo akidai, ameibiwa kura.

error: Content is protected !!