Monday , 26 February 2024
Kimataifa

Rais Trump achunguzwa

Spread the love

Donald Trump, Rais wa Marekani anachunguzuwa na Robert Mueller, ambaye ni mwanasheria maalum kwa kile kinachotajwa kuwa alizuia sheria, kwa mujibu wa gazeti la Washington Post.

Gazeti hilo linaeleza kuwa maafisa watatu wa vyeo vya juu wamekubali kuhojiwa na wachunguzi wa Mueller.

Wakili wa Trump walisema kuwa hatua ya FBI kifichua taarifa kwa gazeti hilo ni kitendo kibaya.

Muller anaongoza uchunguzi wa FBI kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka 2016 na uhusiano wowote wa Trump kwa suala hilo.

Rais Trump mara kwa mara amekuwa akikana kuwa na ushirikiano wowote na Urusi.

Siku ya Jumatano gazeti la washington post lilitaja hatua ya Muller kuchunguza mienendo ya Rais Trump kama hatua kubwa katika uchunguzi huo.

Maafisa ambao hawakutajwa walieleza gazeti hilo kuwa uchunguzi kuhusu Trump kuzuia sheria ulianza siku kadha baada ya Trump kumfuta mkuu wa FBI James Comey tarehe 9 mwezi Mei.

Kabla hajafutwa kzi, Trump alikuwa amepewa hakikisho kutoka kwa Comey kuwa sio yeye alikuwa akichunguzwa.

Hata hivyo Comey tangu wakati huo amedai kuwa Trump amejitahidi kumshawishi aachane na uchunguzi dhidi ya mshauri wake wa masuala ya usalama Machael Flynn.

Flynn alifutwa mwezi Februari kwa kushindwa kufichua kiwango cha uhusiano wake na Sergei Kislyak, ambaye ni balozi wa Urusi nchini Marekani.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!