May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais TLS: Atayechaguliwa asimame imara

Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa TLS anayemaliza muda wake

Spread the love

 

RAIS wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) anayemaliza muda wake, Dk. Rugemeleza Nshala, amesema mgombea yeyote atayechaguliwa kuwa rais wa chama hicho, apiganie misingi ya utawala bora na sheria. Anaripoti Regina Mkonde, Arusha … (endelea).

“Lazima nchi yetu iwe ni jamhuri sio ukiwa rais uwe juu ya sheria, miezi ya karibuni imetokea siwezi kuficha. Mtu akiwa rais ilionekana anaweza kufanya kila kitu, nchi ikiwa na utawala wa sheria kila mtu ataona furaha. Mahakama zitoe maamuzi ya haki zisingiliwe, bunge lisitunge sheria kandamizi,” amesema Dk. Nshala.

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 15 Aprili 2021, wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa TLS unaofanyika jijini Arusha. Chama hicho kinatarajia kufanya uchaguzi wa rais kesho Ijumaa tarehe 16 Aprili 2021, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa jijini Arusha (TLS).

Wagombea watano wa nafasi hiyo ni Dk. Edward Hosea, Flaviana Charles, Shehzada Walli, Francis Stolla na Albert Msando.

Dk. Nshala amesema “suala kubwa ni kuangalia kifungu cha 4 sheria ya TLS kinasema, yale malengo adhimu ya chama hicho ikiwemo kushauri serikali, umma, mahakama na bunge. Kuwasemea watu na kupigania maslahi ya wanachama ni vitu ambavyo chama lazima kipiganie nchi yetu.

“Nawapa rai wenzangu watakaochukua nafasi, waendeleze kupigamia utawala wa sheria na demokrasia kuhakikisha nchi yetu inakuwa na wananchi huru wanaojiamini. Kwa maana hiyo nchi yetu inasonga mbele zaidi,” ameshauri Dk. Nshala.

error: Content is protected !!