April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Shein kufungua mkutano wa Jumuiya ya Madola

Aliyekuwa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein

Spread the love

RAIS wa Zanzibar Dk. Ally Mohamed Shein, anatarajia kufungua mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola, Kanda ya  Afrika tarehe 30 Agosti 30 2019, Visiwani Zanzibar. Anaripoti Danson Kaijage … (endelea).

Hayo amesema Job Ndugai, Spika wa Bunge wakati akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dodoma.

Spika Ndugai amesema Rais huyo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katikamkutano huo utakaohudhuriwa na washiriki takribani 400 mataifa zaidi ya14.

Amesema mpaka sasa spika 20 kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola wamethibitisha kushiriki katika mkutano huo.

Spika Ndugai amesema serikali ya Tanzania itatumia mkutano huo kutangaza vivutio vya utalii pamoja na kuomba washiriki wa mkutano huo kuwekeza katika Jiji la Dodoma.

“Kule tuna kamfuko ketu,tutashawishi na tutaenda na agenda ya tujenge kitega uchumi hapa Dodoma na ni Hoteli ya nyota tano, maana tumekuwa tukikutana na changamoto ya Jiji la Dodoma kutokuwa na Hoteli za nyota tano,”amesema Ndugai.

Hata hivyo, Spika Ndugai amewashauri wafanyabishara kuchangamkia   fursa ya mkutano huo.

“Hivyo naomba kuwashauri wafanyabishara na watanzania wenzangu kwa ujumla fursa hizi tunazipata za kuaminiwa na mataifa mbalimbali tuzichangamkie.Ni fursa adhimu,”amesema na kuongeza.

 “Naomba niseme Bunge letu ni makini na linaaminiwa na ndiyo maana vikao vingine vidogo vidogo vya kamati za hiki chama huwa mara nyingi vinafanyika hapa Tanzania. Hii kwetu ni heshima kubwa kwa weli,”amesema Spika Ndugai.

Kwa upande wake Katibu wa Bunge, Steven Kagaigai  amesema  mpaka sasa maandalizi yote kwa ajili ya mkutano huo yamekamilika ambapo ameaahidi mkutano huo utafanyika kwa usalama wa hali ya juu.

error: Content is protected !!