October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Shein ataja matukio yaliyotikisa utawala wake

Aliyekuwa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein

Spread the love

DAKTARI Ali Shein, Rais wa Awamu ya Saba wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ametaja misukosuko aliyokumbana nayo katika utawala wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Mwaka huu Rais Shein anamaliza muda wake wa vipindi viwili kuiongoza Zanzibar (2010/2015 na 2015/2020), tangu alipoingia madarakani mwezi Novemba 2010.

Akihutubia wakati anavunja shughuli za Baraza la Tisa la Wawakilishi la Zanzibar, leo Jumamosi tarehe 20 Juni 2020, Rais Shein amesema utawala wake uliongoza kwa kuwa upandikizwaji chuki, dharau na uhasama.

Rais Shein amesema katika vipindi vyote viwili vya utawala wake, walikuwepo baadhi ya wananchi waliopandikiza  chuki kwa wenzao, ili kuvunja umoja na kuvuruga amani ya Zanziba.

“Vipindi vyote viwili walikuwepo baadhi ya wananchi wenzetu waliopandikiza chuki ili kuleta fadhaha na  vurugu miongoni mwa watu wamoja wanaopendana, walionesha dharau na kejeli kwa Serikali ili wananchi waichukie, waibeze na waione si serikali yao,” amesema Rais Shein.

Akieleza zaidi juu ya mikasa aliyokumbana nayo, Rais Shein amesema kuna watu waliandaa njama na hila,  ili kuleta mtafaruku.

Hata hivyo, Rais Shein amesema  njama hizo hazikufanikiwa kwa kuwa Mungu aliilinda amani ya Zanzibar.

“Ziliandaliwa njama na hila ili zitokee mtafaruku, lakini kwa uwezo wa mungu ametujalia hali ya amani, umoja, mshikamano na utulivu hadi leo kwa viwango vilevile tulivyokuwa tunatarajia. Tuwe makini na tahadhari kubwa dhidi ya wenye nia mbaya ya serikali yetu, “ amesema Rais Shein.

Rais Shein amesema anamshukuru Mungu kwa kuwa, ametekeleza ahadi yake ya kulinda amani, usalama na utulivu wa Zanzibar, licha ya changamoto alizokumbana nazo.

error: Content is protected !!