November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ziarani Misri

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Jumatano tarehe 10 Novemba 2021, ataondoka nchini kwenda Cairo, nchini Misri kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ziara hiyo, anaifanya kufuatia mwaliko alioupata kutoka kwa Rais wa Misri, Abdel Fattah Al Sisi.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, tarehe 9 Novemba 2021 na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu ya Tanzania imesema, katika ziara hiyo, Rais Samia pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na mwenyeji wake katika maeneo kadhaa ya ushirikiano.

Ushirikiano huo kati ya Tanzania na Misri ikiwemo Nyanja za diplomasia, uchumi, siasa, elimu, utalii na huduma za kijamii.

Haniu amesema, Rais Samian a mwenyeji wake pia, wanatarajia kushuhudia utiaji saini wa mkataba mmoja na hati saba za makubaliano kati ya Tanzania na Misri.

error: Content is protected !!