October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ziarani Marekani

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kesho Jumamosi tarehe 18 Septemba, 2021 anaondoka kwenda New York nchini Marekani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Anakwenda kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 23 anatarajiwa kulihutubia Baraza hilo.

Pamoja na mkutano huo, Rais Samia pia atahudhuria  mikutano ya kilele ya kujadili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)

Aidha, Rais Samia anatarajiwa pia kukutana na Wakuu wa nchi nyingine na viongozi wa Mashirika ya Kimataifa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi na taasisi zao.

Taarifa ya ziara hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 17 Septemba 2021 na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

error: Content is protected !!