Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Rais Samia: Watanzania tusikate tamaa matokeo Taifa Stars
Michezo

Rais Samia: Watanzania tusikate tamaa matokeo Taifa Stars

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amewasihi Watanzania na wadau wote wa soka nchini kutokata tamaa kutokana na matokeo ya Timu ya Taifa (Taifa Stars) kwani bado wana nafasi ya kushinda na kuipa heshima nchi hata tukishika nafasi ya pili. Anaripoti Matilda Buguye, Dar es Salaam  … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Novemba, 2021 Ikulu jijini Dar es salaam wakati akipokea kifimbo cha Malkia wa Uingereza kuashiria uzinduzi michezo ya Jumuiya ya Madola itakayoanza Julai mwaka 2022.

Amewaomba wachezaji, makocha na wadau wote wa timu ya taifa kutokata tamaa badala yake kuinuka na kurekebisha kasoro na kuendelea kilipigania Taifa.

“Niseme kidogo kuhusu Taifa Stars, ni kweli tumepoteza juzi lakini hatujapoteza matumaini. Niwaase Watanzania tusikate tamaa bado tuna nafasi ya kushinda na kuipa heshima nchi yetu hata tukishika nafasi ya pili.

Rais Samia Suluhu Hassan

“Nampongeza Waziri Mkuu, Wizara ya Michezo, TFF, wachezaji na Watanzania wote kwani niliona hali na hamasa kubwa sana kuelekea mechi dhidi ya DR Congo ambapo Watanzania kwa ujumla walijaa uwanjani, lakini mchezo ni mchezo tulijipanga vizuri lakini bahati haikuwa yetu,” amesema.

Akizungumzia kifimbo hicho, Rais Samia amesema Tanzania imekuwa ni mwanachama na mshiriki mzuri wa michuano ya Jumuiya ya Madola tangu ilipoanza kushiriki mwaka 1962 na kushinda medali 21 ambazo kati ya hizo sita za dhahabu, sita za fedha na tisa za shaba.

“Nitoe wito kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya michuano ya Jumuiya ya Madola kuhakikisha tunazirudisha medali zetu ambazo zimepotea kwa muda sasa.

“Ujio wa kifimbo hiki hapa nchini ni wa mara ya saba. Kifimbo hiki (cha Malkia) ujio wake uwe ni kengele ya kutuamsha kuhusu ushiriki wetu na kufanya vizuri” amesema.

Mapema tarehe 11 Novemba, 2021, Timu ya Taifa stars iliambulia kipigo cha mabao 3 -0 kutoka kwa Timu ya Taifa ya Congo DRC katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars kwa sasa imesafiri kwenda nchini Madagascar kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano hapo kesho saa 10 kamili jioni

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!