Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia: Tutaendelea kukopa, tumalize miradi yote
Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia: Tutaendelea kukopa, tumalize miradi yote

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema, Serikali anayoingoza itaendelea kukopa mikopo ya masharti nafuu ili kuendeleza na kuanzisha miradi mingine mipya ya maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne, tarehe 28 Desemba 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokuwa akishuhudia utiaji saini wa ujenzi wa awamu ya tatu wa reli ya kisasa (SGR) kati Makutopora- Tabora yenye urefu wa kilomita 368, wenye thamani ya Sh.4.4 trilioni. Itajengwa kwa miezi 46

Amesema, alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, baada ya kifo cha aliyekuwa Rais, John Pombe Magufuli, aliahidi kuendeleza miradi yote iliyokuwapo na kuanzisha mipya na hilo atahakikisha linafikiwa ikiwemo ujenzi wa SGR na Bwana la Umeme la Julius Nyerere.

“Kama walidhani kutakuwa na kusimamisha miradi wapate la kusema halipo, halipo na kuna jitihada za kutuvunja mioyo kwenye mikopo, hata nchi zilizoendelea zinakopa, tutakopa kwani ukikopa unajenga haraka na mikopo hii ni ya miaka 20, kwa hiyo tutakopa na tutalipa taratibu,” amesema Rais Samia

Amesema, tukiweza kuiunganisha na nchi zote zinazotuzunguka, uchumi wetu utakua sana kwani tutakuwa na njia za kwenda kokote. Wizara hakikisheni mnakamilisha hili na lengo ni kuifanya nchi yetu inakuwa kitovu cha biashara.

“Wale wanaosema mkopo ni kurudi nyuma inategemea unaitumiaje, hata kwenye halmashauri kuna wanaochukua mikopo wanakwenda kufanya maendeleo na wengine wakifika nyumbani baba anaichukua anakwenda kupiga ulanzi. Sasa kabla ya kusema jiulize mkopo unachukuliwa unakwenda kufanya nini,” amesema

Aidha, ametumia fursa hiyo kuwataka wasimamizi wa reli hiyo kuhakikisha, “ubora wa vifaa vinavyonunuliwa uendane na reli inayojengwa kwa sababu
miezi michache niliyokaa serikali, nimeona mambo mengi sana ambayo huko nyuma yalikuwa hayafanyiki lakini sasa yanataka kufanyika, sitakubaki yafanyike.”

“Niwaombe sana wanaosimamia ujenzi wa reli, wahakikishe inakuwa yenye viwango na ijengwe kama inavyokusudiwa. Hizi ni fedha za Watanzania, tusifanye vitu kwa ubora. Hata ikiharibika miaka mitatu na mkandarasi kaondoka, tutashikana,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!