Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Tunataka  Kigoma iwe kitovu cha biashara
Habari za Siasa

Rais Samia: Tunataka  Kigoma iwe kitovu cha biashara

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake inataka kuurejesha Mkoa wa Kigoma katika hadhi ya kitovu cha biashara kwa kufungua fursa za kibiashara kati ya mkoa huo na nchi jirani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Rais Samia ametoa ahadi hiyo leo Jumanne, tarehe 18 Oktoba 2022, akizungumza na wananchi wa mkoa huo, akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa Bandari ndogo ya Kibirizi, mkoani Kigoma.

Amesema, Serikali yake imeamua kuijenga bandari hiyo kisasa ili biashara kati ya Tanzania na nchi jirani zinazopakana na Kigoma, zifanyike kwa ufanisi mkubwa.

“Tunafanya hivyo kwa sababu tunataka kuirejesha Kigoma kuwa kitovu cha biashara, ndiyo maana mambo meni tunaleta sasa hivi Kigoma. Tunajenga bandari, umeme wa kutosha tunaleta ili watu waweze kufanya biashara vizuri, wawekezaji waje na mambo mengine,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amemuagiza Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kuusadia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA),kujenga barabara inayoingia bandarini hapo.

Huku akiuagiza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na uongozi wa wafanyabiashara wadogo, kujenga upya vibanda vya biashara vilivyo karibu na eneo la bandari.

“Nakwenda kutafuta fedha za kujenga eneo hilo naomba nanyi muanze kujipanga, mjipange kupitia umoja wenu wa wafanyabiashara, tukubaliane jinsi patakavyotengenezwa hapo ili mtu akitoka bandarini pazuri akute na wafanyabiashara wamekaa pazuri na biashara inaendelea,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!