May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Tunafufua mradi Bandari Bagamoyo

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema, serikali imeanza mazungumzo ya kufufua mradi wa Bandari ya Bagamoyo pamoja na ule wa Mchuchuma na Liganga. Anaripti Yusuph Katimba, Dar es Salaam…(endelea).

“Tumeanza mazungumzo ya kufufua Mradi wa Bagamoyo (Bandari ya Bagamoyo), pamoja na Mradi wa Mchuchuma na Liganga. Tunaenda kufanya mazungumzoa na taasisi iliyokuja ili mradi wa Bagamoyo tuufungue, amesema Rais Samia.

Rais huyo ametoa kauli hiyo leo tarehe 26 Juni 2021, wakati akizungumza katika Mkutano 12 wa Baraza la Taifa la Biashara, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo utaendelea baada ya mazungumzo na taasisi husika ambayo tangu awali ndiyo ilikuwa ikianza mchakato wake.

Katika miaka sita iliyopita, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ulikuwa ukitajwa kama mmoja wa miradi ya kimkakati wenye fursa kubwa ya kuzimua uchumi midomoni kwa watumishi wa umma na viongozi wa serikali.

Hata hivyo, baada ya Hayati Rais John Magufuli kungia madarakani na kuanza kuzungumzia mradi huo, alikuwa akisema ulikuwa na masharti ya hovyo ambayo serikali yake isingeweza kuyakubali.

Kauli hiyo kutoka kwa Rais Magufuli ilizua mkanganyiko miongoni mwa wananchi; wengine wakiamini wale waliosema bandari hiyo ijengwe na wengine wakiamini mradi huo ni wa hovyo.

Maneno ya Rais Magufuli yalikuja katika wakati ambao kulikuwa na taarifa nyingi kuhusu namna China inavyotwaa mali zisizohamishika za nchi zilizokopa fedha kutoka kwake na zikashindwa kurejesha kwa wakati. Mifano uliokuwa ukitolewa ulihusu nchi kama Zambia na Sri Lanka.

Katika mkutano wake na wafanyabiashara nchini, Rais Magufuli alizungumza waziwazi kwamba, kwa namna makubaliano yale ya Tanzania na wawekezaji yalivyokuwa, mkataba ule ulikuwa hauna maslahi na Tanzania, naye asingekubali kuona mradi huo ukiendelea kwa namna hiyo.

“Yaani kwenye eneo lote kuanzia Tanga hadi Mtwara kusijengwe bandari yoyote. Bandari ya Kilwa tusiiendeleze, Bandari ya Mtwara ambayo itawezesha Mikoa ya Kusini kupokea mafuta badala ya Dar es Salaam kisha yarudihuko, hatutakiwi kuiendeleza, barabara kutoka Mtwara hadi Bamba Bay ambayo itatuwezesha kusafirisha mizigo hadi Msumbiji tusiijenge,” alidai Rais Magufuli.

Hata hivyo, Hiyo ndiyo Tanzania ambayo Rais Samia imeamua kuendeleza mradi huo kwa maelezo una manufaa makubwa katika nchi.

Akizungumzia mradi wa Mchuchuma na Liganga, Rais Samia amesema tayari ametoa maelezo ili kuangalia palepalipo na tatizo na kwamba, duniani kwa sasa chuma kimepanda bei.

error: Content is protected !!