October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Trilioni 1.3 zibaki, kilio wakandarasa sasa basi

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ameagiza watekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa shule na maji nchini, kuwatumia wakandarasi wa ndani kwa kuwa miaka mingi wamekuwa wakilia kutopata zabuni kutoka serikalini. Anaripoti Mwandishi wetu (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Oktoba, 2021 jijini Dodoma wakati akizindua kampeni ya maendeleo kwa ustawi na mapambano ya UVIKO -19 ambao umetokana na mkopo nafuu wa Sh trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika hilo la IMF.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha fedha hizo zinabaki nchini.

“Zinapaswa kuzunguka ndani ya uchumi wa nchi hapa na zisitoke nje.

“Wakandarasi sasa kazi hizi hapa, tunaomba sana wenyewe wakawe wakandarasi wenye sifa, wakandarasi bora ambao watafanya kazi kwa umakini, ufanisi na uwajibikaji mkubwa. Nawatetea ili fedha hii ilipwe kwao iweze kuzunguke kwenye uchumi wa hapa nchini,” amesema.

Pia ametoa rai kwa wasimamizi wa miradi hiyo kwamba wazingatie muda wa utekelezaji wa program hiyo ambayo ni miezi tisa.

error: Content is protected !!