RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la nchi hiyo, Job Ndugai. Anaripoti Matilda Peter, Dodoma … (endelea).
Mazungumzo hayo, yamefanyika leo Jumanne, tarehe 20 Aprili 2020, Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
Rais Samia, amefanya mazungumzo na kiongozi huyo wa Bunge, ikiwa ni siku moja imesalia, kabla ya kulihutubia Bunge.
Keshokutwa Alhamisi, Rais Samia atakihutubia Bunge la Tanzania, kwa mara ya kwanza, tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021.
Iliingia madarakani baada ya aliyekuwa Rais John Pombe Magufuli, kufariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam na mwili wake, kuzikwa nyumbani wake, Chato mkoani Geita.
Bunge hilo la 12, lilizinduliwa na Hayati Magufuli tarehe 13 Novemba 2020.
Leave a comment