May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Siku 100 za uhuru mahakamani

Spread the love

 

TAREHE 27 Juni 2021, Rais Samia Suluhu Hassan atatimiza miaka 100 akiwa madarakani. Aliapishwa 19 Machi 2021, baada ya mtangulizi wake Rais John Magufuli kufariki dunia. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Katika kipindi hicho, Rais Samia amebadili mtazamo wa Watanzania katika suala la utoaji haki kupitia mahakama. Tabia yake ya kupenda haki imedhihiri wazi.

Hiii ni kutokana na mwongozi wake kwa wateule na watendaji wa mahakama kusimamia misingi ya kikatiba katika kusikiliza na kufikia tamati kwenye kesi za watuhumiwa kulingana na sheria za nchi.

Katika siku 100 za Rais Samia, Tanzania imeshuhudia matukio makubwa kadhaa ikiwa ni pamoja na kuachwa huru viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI).

Viongozi hao walikaa mahabusu kwa zaidi ya miaka minane, wakikabiliwa na tuhuma za ugaidi katika Kesi ya Jinai Na. 121/2021. Muda wote huo kesi zao hazikuwa zikisikilizwa, hata walipoomba kusikilizwa, ombo lao halikutekelezwa.

Ndani ya siku 100 za Rais Samia, kesi hizi zimesikilizwa na kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu, kesi hizo zilifutwa.

Ndani ya siku 100 za Rais Samia madarakani, Tanzania imeshuhudia kwa mara ya kwanza aliyekuwa Mkuu wa Wilaya kufikishwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo unyang’anyi kwa kutumia silaha. Ni Lengai Ole Sabaya (Hai).

Mvumo wa Sabaya na wenzake – Sylvester Nyegu, Wadson Stanley, Enock Togolan, John Odemba na Daniel Mbura – ulitokana na vitendo vyako ambavyo hakuwekwa wazi katika utawala wa Awamu ya Tani chini ya Dk. Magufuli.

Ukubwa wa tuhuma zake ulidhihiri ndani ya siku 100 za Rais Samia baada ya Sabaya (34) kufikishwa mahakamani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Arusha tarehe 4 Juni 2021.

Habinder Sethi, mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) anakuwa kilelezao cha haki ndani ya siku 100 za Rais Samia madarakani.

Kiu yake ya kutaka kuungana na familia yake tangu mwaka 2017 alipowekwa mahabusi kwa tuhuma za uhujumu uchumi pamoja na wenzake wawili, Mfanyabiashara James Rugemalila.

Seth alikiri na kukubali kulipa Sh. 26.9 bilioni ndani ya miezi 12, kupitia makubaliano ya kisheria (Plea Bargain), aliyofanya na DPP Mwakitalu.

Pia siku 100 za Rais Samia zimeitekenya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) ambapo imefuta kesi 147 zilizokosa Ushahidi. Maagizo hayo yalitoka kwa Rais Samia.

Siku 100 za Rais Samia zimetosha kumfutiwa mashtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi wa Logistik, Byekwaso Tabura.

Laurean Rugambwa Bwanakunu, aliyekuwa Mkurugenzi wa MSD

Bwanakunu na mwenzake walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano, ikiwemo kuisababisha MSD hasara ya Sh. 3.8 bilioni na kutakatisha fedha kiasi cha Sh. 1.6 bilioni. Ushahidi wake haukuonekana.

Marijan Msofe ‘Papa Msofe,’ ni mfanyabiashara ambaye ameonja ladha ya siku 100 za Rais Samia katika msukumo wa uamuzi ake kuhusu kesi zisizo na Ushahidi.

Papa Msofe na wenzake wanne, Wenceslaus Mtu, Mwesiga Mhingo, Josephine Haule na Fadhili Mganga walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumi uchumi katka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Sasa yupo huru.

error: Content is protected !!