May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Polisi tumieni Tehama kudhibiti uhalifu

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amelitaka jeshi la polisi kujipanga vizuri kwenye masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) ili kudhibiti matukio ya uhalifu kikamilifu. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah TUDARCo … (endelea).

Rais Samia ametoa maagizo hayo leo Jumatano tarehe 25 Agosti 2021 wakati akifungua kikao kazi cha maofisa wakuu waandamizi wa jeshi la polisi na makamanda wa polisi wa mikoa/vikosi – Oysterbay Dar es salaam.

Amesema katika siku za karibuni masuala ya uhalifu yamekuwa yakihusisha teknolojia hususani matukio ya wizi kwa njia ya mtandao.

Pia, amesema Tehama hutumiwa zaidi na wahalifu wa ugaidi hivyo ni vema jeshi la polisi nalo likabadilika na kujiimarisha katika matumizi ya Tehama ili kubaini wahalifu hao kwa urahisi.

Aidha, ameliagiza jeshi hilo kukemea na kuwakamata wafanyabiashara wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

error: Content is protected !!