Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Nafahamu madhara ya kubadili viongozi mara kwa mara
Habari za Siasa

Rais Samia: Nafahamu madhara ya kubadili viongozi mara kwa mara

Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema hana lengo na hapendi kubadilisha viongozi mara kwa mara kwa kuwa anafahamu madhara yake, ikiwemo kuchukua muda mrefu kuwajenga viongozi wapya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kiongozi huyo wa Tanzania, ametoa kauli hiyo akifungua semina elekezi kwa mawaziri, manaibu waziri, makatibu na manaibu katibu wakuu, leo tarehe 2 Machi 2023, jijini Arusha.

“Mimi sio lengo langu kubadilisha viongozi mara kwa mara, kwa kuwa huchukua muda mrefu kuwajenga. Hata hivyo, wakati mwingine nalazimika kufanya hivyo ili kuepusha madhara zaidi serikalini na kwa wananchi,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “ninafahamu madhara ya kubadilisha viongozi mara kwa mara na huwa sipendi kufanya hivyo sababu kunafanya watu wafanye kazi kwa hofu na viongozi wasiwe na mipango ya muda mrefu kwa kuhofia teuzi zao kutenguliwa. Kiongozi anapoondoshwa kazini ni fedheha kwa familia yake na watoto ambao walikuwa wanamuona mtu wa mfano.”

Akizungumzia semina hiyo elekezi, Rais Samia amesema kutokufanyika kwake mara kwa mara, kumeleta athari serikalini kwa kutengeneza ombwe la uelewa wa taratibu za utendaji kazi.

“Kutokufanyika kwa mikutano kama hii kwa muda mrefu kumeleta athari zinazoonekana wazi katika utendaji serikalini, kumekuwepo na ombwe la uelewa wa taratibu za utendaji kazi serikalini na hii ni moja ya sababu ya viongozi kubadilishwa mara kwa mara, ili kuepusha serikali na fedheha ya kuwa na viongozi wanaozifanya wizara kuwa sehemu ya malumbano na migawanyiko isiyo na tija,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amewataka washiriki kuutumia mkutano wao wa faragha kujadili namna ya kuboresha uongozi bora.

“Mwalimu Nyerere alitueleza ili taifa letu liendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Watu tunao, siasa safi ipo sababu tunapotoka nje ya nchi sifa tunazopata ni kutokana na siasa safi tuliyo nayo. Suala la uongozi bora sasa haliko, tutakwenda kulijadili hapa,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!