May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Mwendo ni ule ule

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema, wale wanaodhani usimamizi wa rasilimali za nchi, ukwepaji kodi, rushwa vimekwenda na Hayati John Magufuli, wanajidanganya. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

“Naomba nitumie jukwaa la Bunge kusema mambo mawili madogo, kuwaonya wale wote wanaodhani kuwa usimamizi wa mali za umma, ukwepaji kodi, uzibaji mianya ya kupoteza mapato, kukemea uzembe na wizi yameondoka na Hayati Magufuli.

“Spika (Job Ndugai) nataka niseme, Hayati Magufuli amekwenda peke yake, na kama nilivyosema siku ile tunamsindikiza, maono falsaa na mikakati aliyotuachia, tunaendelea kuyafanyia kazi. Hivyo basi, wale wanaodhani yale amekwenda nayo, wamejidanganya. Yapo na tunayatekeleza,” amesema.

Kiongozi huyo wan chi ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma wakati akihutubia bunge hilo kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kwake tarehe 19 Aprili 2021.

Amesema, ameamua kutoa kuali hiyo kwa kuwa, kuna baadhi ya watu wameanza kulegalega kwenye utendaji kazi na kwamba, wizi umeanza kushamiri katika baadhi ya maeneo.

“…lakini kuna wawekezaji waliokuwa na nia nzuri ya majadiliano na serikali, wamerudi nyuma. Nataka kuwamabia, mwendo ni ule ule,” amesema.

error: Content is protected !!